Wajasiliamali wilayani Ileje mkoani Songwe watakiwa kutumia mitandao ya kijamii kutangaza biashara zao Kwa lengo la kupata wateja wenye uhitaji wa bidhaa zao.
Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Farida Mgomi amesema hayo Julai 9, 2023 wakati akizungumza na wafanyabiashara wajasiliamali wadogo wadogo katika ukumbi wa CCM wilayani hapo katika kikao kilichoandaliwa na jumuiya ya vijana wa chama hicho wenye lengo la kuhamasisha vijana kufanya biashara zao kwa ushirikiano kati ya sekta binafsi na serikali.
Mgomi amewataka vijana kufanya biashara kulingana na wakati uliopo kutokana na kukua Kwa sayansi na teknolojia kufungua akaunti za motandao ya kijamii kama WhatsApp, Instagram na Twitter ili kuhakikisha wanajipatia kipato kupitia mitandao.
Mgomi amewataka vijana kuendelea kujifunza namna ya kutumia teknolojia ya kufanya biashara kwenye maeneo Yao sambamba na kuomba mikopo Ya asilimia 10, Kwa vijana 4% ,wanawake 4% na makundi maalaumu 2% isiyo na riba kwenye halmashauri Ili kukuza mitaji ya biashara zao.
Mgomi amewataka vijana kujiunga pia kwenye vyama vya wafanyabiasha ambako huandaliwa jukwaa la kuwasilisha changamoto kupitia sekta binafai zinazowakabili kwenye biashara zao na kuzipatia ufumbuzi.
Mgomi amewasihi vijana kujiunga na vyama vya wafanyabiashara Tanzania ambavyo ni vyama vya Wafanyabiashara kama TCCIA,Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) , TWCC kwani vimekuwa kinara katika majadiliano kati ya Serikali na Sekta Binafsi.
Mwenyekiti wa jumuiya ya vijana wilayani humo Diana Ngabo amesema lengo la kuandaa hafla hiyo ni kuyatambua aina ya makundi ya vijana na kuwasilisha changamoto zinazowakabili mbele ya mkuu wa wilaya Ili ziweze kutatuliwa.
Katibu wa siasa na uenezi wilaya ya Ileje Maoni Mbuba akizungumza katika kikao hicho amewasihi vijana kuwa wazalendo na waminifu Kwenye biashara Zao na kutosita kuwasilisha changamoto wanazokabiliana nazo katika shughulizi zao za Kila siku ili zipatiwe ufumbuzi.