Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DART yatoa suluhu maalum maonesho ya Sabasaba Dar

IMG 20220629 WA0017 DART yatoa suluhu maalum maonesho ya Sabasaba Dar

Wed, 29 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Tawala wa Mkoa Dar es Salaam Hassan Rugwa amesema Wakala wa Mabasi yaendayo haraka (DART) imetoa suluhu ya usafiri kwa maalum katika kipindi cha maonyesho ya biashara Kimataifa yanayofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere (Sabasaba).

Rugwa ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati uzinduzi wa safari maalum mabasi yaendayo haraka katika maonesho ya sabasaba kwani imerahisisha usafiri kwa wananchi pamoja na wafanyabiashara kwa kipindi cha sabasaba.

Amesema huduma ya usafiri ni changamoto katika kipindi cha maonesho hivyo DART imeona hilo mbalimbali katika kusaidia wananchi kupata usafiri wa uhakika wakiwa katika maonesho.

Nae Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Deus Kasmir amesema DART imejipanga katika kutoa huduma ya usafiri katika kipindi cha maonesho ya sabasaba kwani wanatambua idadi kubwa ya ambao wanahitaji kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine.

Amesema katika hiki wananchi wanaokwenda katika maonesho ya sabasaba wasifikiri suala la usafiri kwani usafiri upo katika safari za mbagala hadi viwanja vya sabasaba na Gerezani Sabasaba

Chanzo: www.tanzaniaweb.live