Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DART sasa kuendeshwa kwa ubia

Mwendokasipic DART sasa kuendeshwa kwa ubia

Wed, 15 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo kwa njia ya ubia (PPP), Serikali imesema miradi mitano ipo katika hatua ya ununuzi wa mbia ikiwemo Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart) awamu ya kwanza.

Hayo yameelezwa leo Juni 14,2022 jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba wakati akiwasilisha akiwasilisha bungeni mapendekezo ya Serikali ya makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2022/23 huku akieleza hatua hiyo inalenga kuipa nafasi sekta binafsi kuongeza ufanisi wa uendeshaji na utoaji wa huduma.

Waziri huyo amesema mradi huo hadi sasa umeshapata mbia wa uendeshaji ambapo hatua inayofuata ni majadiliano na mbia huyo.

“Hatua hii itaongeza ufanisi wa uendeshaji na utoaji wa huduma na mradi huu utakuwa mradi wa kielelezo uliopitia hatua zote zinazotakiwa kwa mujibu wa Sheria ya PPP, Sura 103.

“Upatikanaji wa wabia katika miradi ya PPP utaleta ahueni katika bajeti ya Serikali na hivyo kuwezesha kuongeza rasilimali fedha katika maeneo mengine na hivyo kuwaletea maendeleo watanzania,”

Amesema Serikali itaendelea kufanya tathmini ili kuboresha na kuipa nafasi sekta binafsi kushiriki katika kutekeleza miradi ya Serikali kwa mfumo wa Ubia na hivyo Serikali kujikita zaidi katika kuweka mazingira wezeshi na kuboresha huduma za kijamii

Chanzo: www.tanzaniaweb.live