Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Covid-19 yaifanya TRA kujikita katika tehama

39cc8b22ecce687c0c6c74d879a44c2f Covid-19 yaifanya TRA kujikita katika tehama

Mon, 6 Sep 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

CHANGAMOTO ya ugonjwa wa Covid-19 umeifanya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kufanya kazi kwa kutumia mitandao zaidi ili kupunguza msongamano itakayosababisha maambukizi.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo alisema hayo wakati akifungua semina ya Klabu ya Waandishi wa Habari Dar es Salaam(DCPC) iliyoandaliwa na mamlaka hiyo.

Kayombo alisema ndani ya miaka miwili hii dunia imekumbwa na Covid-19 na kuifanya jamii kubadilisha njia ilizozoea katika utendaji wa shughuli zao; ndio maana mamlaka hiyo ikajikita zaidi kwenye njia za tehama.

“Hivi sasa upatikanaji wa TIN ni kwa njia ya mtandao ili mhitaji apate akiwa sehemu yoyote cha msingi mtu awe na namba ya NIDA(Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa).

“Tulianzisha utaratibu wa minada kwa njia ya mitandao, awali kwenye minada kulikuwa na changamoto wanaoshiriki ni wale wale hasa Dar es Salaam, tukaamua kuanza kieletroniki kuongeza ufanisi, utendaji na ushindanaji wa haki,”alisema.

Pia Kayombo alisema mamlaka hiyo na wanahabari kuna jambo linawaunganisha, lakini pia ipo kwa ajili ya kutumikia watanzania katika ukusanyaji wa mapato.

Alisema TRA Katika kutekeleza majukumu yao kila wakati imekuwa ikikutana na walipakodi kutoa elimu katika kuwakumbusha haki yao na wajibu wao.

Awali Mwenyekiti wa DCPC, Irene Mark alisema semina hiyo itatoa mwanga kwa wanahabari kuhusu tozo mbalimbali, lengo likiwa ni kupata ufafanuzi kwa kuwa katika siku za karibuni serikali imekuwa ikitilia mkazo kuhusu tozo.

Alisema klabu hiyo mpaka sasa ina wanachama 120 ambayo ina lengo la kuwaunganisha waandishi wa habari na wadau wengine mbalimbali.

Chanzo: www.habarileo.co.tz