Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Corona yaacha maumivu sekta ya Bima

Magari Mapato yatokanayo na Bima ya magari yashuka Tanzania

Mon, 9 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Licha ya serikali ya Tanzania kutokuweka masharti ya kutotoka nje kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19 kama Mataifa mengine ya Afrika ya Mashariki Takwimu zinaonyesha bado sekta ya Bima imeathirika na mlipuko wa ugonjwa huo.

Mapato yatokanayo na biashara ya Bima yameanguka kwa asilimia 1.6 kwa mwaka 2020 ukilinganisha na mwaka 2019, hali hiyo inasemekana imechochewa na kuanguka kwa biashara ya utalii na miradi ya baharini na uhandisi.

Ripoti iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Bima Tanzania (Tira) imedai kushuka kwa shughuli za baharini kumeongeza kuzorota kwa biashara hiyo ukilinganisha na mwaka 2019.

"Hali hii kwa kiasi kikubwa imesababisha na katazo la kuzuia watu kutoka nje kwa baadhi ya mataifa ambayo moja kwa moja iliathiri miradi mikubwa ya baharini na uhandisi nchini Tanzania".

Kwa Mujibu wa taarifa iliyotolewa na Tira imedai, Malipo makubwa ya bima yalishuka kwa kiasi cha shilingi bilioni 689 kwa mwaka 2020 ukilinganisha na bilioni 694 mwanzoni mwa mwaka 2020 hadi decemba 31 2021.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live