Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Corona haiwatishi Watalii Kutoka Israel

Watalii Pcc Data Watalii kutoka Israel

Mon, 2 Aug 2021 Chanzo: Mwananchi

Kundi la watalii 150 kutoka nchini Israel limetua uwanja wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) leo Agosti 2 saa 10:30 alfajiri kwa ajili ya kutembelea hifadhi za taifa.

Watalii hao ni sehemu ya watalii 900 ambao wanatarajia kutua nchini mwezi huu kutembelea vivutio vya utalii.

Akizugumza baada ya kupokea watalii hao Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela amesema ujio wa watalii hao ni kutokana na kazi nzuri ya kutangaza utalii inayofanywa na serikali na wadau wa utalii.

"Leo tumepokea kundi la kwanza la watalii hawa ambao wanakuja nchini kipindi hiki ambacho dunia inakabiliwa na janga la Corona," amesema RC Mongela.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mawasiliano wa shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA), Pascal Shelutete amesema ujio wa watalii hawo ni jitihada kubwa za kutangaza Utalii katika masoko mapya, ikiwepo Israel ambayo imechangiwa pia na serikali kufungua ubalozi nchini humo.

Shelutete pia amesema watalii hao watatembelea hifadhi za kaskazini na Mamlaka ya hifadhi Ngorongoro.

Soko jipya la Watalii kutoka Israel limeonekana kuwa zuri kwani mwaka jana pia Tanzania ilipokea zaidi ya watalii 1000.

Chanzo: Mwananchi