Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Coaster zaruhusiwa kubeba abiria Ubungo

89482 COSTAPIC Coaster zaruhusiwa kubeba abiria Ubungo

Sat, 21 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (Latra) imeruhusu magari madogo ya abiria aina ya Coaster kubeba abiria kutoka Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam kwenda mikoani.

Licha ya kutoa vibali hivyo, baadhi ya wamiliki wa magari hayo wameshindwa kukamilisha taratibu ili kupewa vibali.

Akizungumza na Mwananchi ofisa leseni wa Latra, Leo Ngowi amesema wameanza kutoa leseni hizo za muda kutokana na kuongezeka kwa abiria, wengi kukosa usafiri jambo linalosababisha usumbufu.

"Tumeruhusu Coaster na gari nyingine binafsi zenye uwezo wa kubeba abiria kusaidia idadi kubwa ya wasafiri wanaokwenda mikoani katika sikukuu za mwisho wa mwaka,” amesema Ngowi.

Amesema ili kibali kitolewe ni lazima gari husika lifungwe kifaa maalum.

Chanzo: mwananchi.co.tz