Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chupa kubwa zaidi duniani yauzwa kwa Tsh bil 32

World Largest Scotch Fails To Break Record FT BLOG0522 Chupa kubwa zaidi duniani yauzwa kwa Tsh bil 32

Sat, 4 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Taarifa ikufikie kuwa, chupa kubwa zaidi duniani ya whisky, yenye na ujazo wa lita 311 imeuzwa kwa zaidi ya Tsh bilioni 31.89.

Chupa hiyo iliyopewa jina la ‘The Intrepid’ ina urefu wa futi 5, na mwaka wa 2021 iliingia katika rekodi ya Dunia ya Guinness ya whisky kubwa duniani.

‘The Intrepid’ ina chupa 444 za kawaida, sawa na galoni 68.41, zenye thamani ya whisky. Chupa hiyo iliyovunja rekodi ya dunia iliuzwa kwa mnada mnamo Jumatano, Mei 25, kwa mnunuzi asiyejulikana.

Seti kadhaa za chupa za kipekee na picha ndogo za whisky sawa iliyotumiwa katika Intrepid pia ziliuzwa.

“Sote tumefurahishwa na matokeo haya. Katika kipindi cha miaka miwili na nusu iliyopita, chupa hii kubwa na kila kitu inachosimamia imetuwezesha kupata fursa nyingi.

Shukrani ziwaendee wavumbuzi 11, na tunatumaini wamefaidika kwa kuwa sehemu ya mradi huu,” alisema Jon Land, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Rosewin Holdings.

Pombe ya chupa hiyo ilitengenezwa na The Macallan huko Speyside, Scotland, mwaka wa 1989, hii ni kwa mujibu wa nyumba ya makumbushio ya Lyon na Turnbull.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live