Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chuo cha Kodi chajivua kuzalisha wataalam waliobobea

Chuo cha Kodi chajivua kuzalisha wataalam waliobobea

Sat, 23 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati Chuo cha Kodi nchini Tanzania kikifanya mahafali ya 12 kesho Ijumaa Novemba 22, 2019, uongozi wa chuo hicho unajivunia kuzalisha wataalam waliobobea katika masuala ya kodi na forodha.

Mkuu wa chuo hicho,  Profesa Isaya Jairo amesema  wahitimu 417 wanatarajia kuhitimu mwaka 2019 na wameandaliwa vya kutosha katika fani hizo.

Amesema wahitimu hao watatunikiwa vyeti na Waziri wa Fedha na Mipango,  Dk Philip Mpango atakayekuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo.

Amesema  wahitimu hao watatunukiwa vyeti vya stashahada na shahada za kozi mbalimbali zinazotolewa chuoni hapo.

“Mahafali haya ya 12 yanafanyika wakati chuo kinajivunia mafanikio mengi katika mafunzo ya forodha na kodi kwa miaka 12 huku kikiwa ni chuo pekee nchini na katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kusini chenye usajili na ithibati ya kudumu kutoa mafunzo ya Forodha na kodi kwa wadau mbalimbali.”

“Katika mahafali hayo wahitimu 132 watatunukiwa cheti cha Uwakala wa Forodha cha Afrika Mashariki (EACFFPC) huku wahitimu 23 wakitunukiwa cheti cha Usimamizi wa Forodha na Kodi (CCTM) na wahitimu 60 watatunukiwa Stashahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi (DCTM),” amesema  Profesa Jairo.

Ameongeza kuwa wahitimu 177 wanatarajiwa kutunukiwa vyeti vya Shahada ya Usimamizi wa Forodha na Kodi (BCTM) na  25 wakitarajia kutunukiwa vyeti vya Stashahada ya Uzamili katika kodi (PGDT).

Amesema  kuwa chuo kimekuwa na mikakati mbalimbali ya kuhakikisha udahili wa wanafunzi chuoni hapo unaongezeka.

Chanzo: mwananchi.co.tz