Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Choroko yaongezeka bei

869fdf6e7937c6c21563810035d84fd1 Choroko yaongezeka bei

Sun, 14 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

BEI la zao la choroko mkoani hapa limepanda kutoka Sh 1,493 kwa kilo moja na kufika bei ya Sh 1,623.

Hayo yalisemwa na Meneja Shughuli wa Chama Kikuu cha Ushirika Nyanza (NCU), John Masalu wakati wa mahojiano malumu na gazeti hili.

“Mkoa wa Mwanza umeanza mnada wa pili sasa, katika mnada wa kwanza jumla ya tani 47 ziliuzwa na bei ilikuwa 1,493. Katika mnada wa pili jumla ya tani 47 imeuzwa kwa bei ya shilingi 1,623,” alisema Masalu.

Alisema bei ya 1,623 imekuwa kubwa na haijawahi kutokea tangu enzi za Uhuru na kuongeza kuwa katika mnada wa tatu wa zao hilo ana amini tani za choroko zitakuwa nyingi sana.

Masalu alisema kupanda kwa bei kutahamasisha wakulima kupelekea zao la choroko kwa vyama vya ushirika (AMCOS) na kuwa wakulima watakuwa wakilipwa malipo yao ndani ya saa 48 na kupitia akaunti ya benki.

Alisema kwa wakulima ambao hawana akaunti malipo yao yatafanyika kupitia simu zao za mkononi.

Chanzo: habarileo.co.tz