Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

China yatoa tani 2,396 za mchele

Mchele Nchi Jirani China yatoa tani 2,396 za mchele

Wed, 17 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya China kupitia ubalozi wake nchini Sudan Kusini, imetoa tani 2,396 za mchele kusaidia wakimbizi na watu walio katika mazingira magumu nchini hapa.

Balozi wa China nchini Sudan Kusini, Ma Qiang alisema mchango huo wa mchele umelenga kusaidia watu wanaokabiliwa na uhaba wa chakula unaosababishwa hasa na majanga ya asili na mzozo wa hivi karibuni nchini Sudan.

“Ni furaha yangu kuikabidhi serikali tani 2,396 za mchele,” alisema na kuongeza kuwa, Sudan Kusini inakabiliwa na changamoto za uhaba wa chakula kutokana na majanga ya asili kama vile mafuriko na tauni ya nzige.

Kwa mujibu wa Qiang, zaidi ya watu 50,000 waliokimbia ghasia nchini Sudan wamewasili Sudan Kusini.

“Sehemu ya mchele uliotolewa na China itagawiwa kwa watu hawa wanaorejea ili kukidhi mahitaji yao ya dharura,” alisema.

Waziri wa Masuala ya Kibinadamu, Albino Akol Atak alisema mchango huo umekuja wakati sahihi kwani nchi inakabiliwa na watu wengi wanaokimbia machafuko nchini Sudan.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live