Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

China yashikiria msimamo wake wa 'uwazi kwenye biashara'

China Itafanya Mazoezi Ya Kijeshi Kupambana Na Ugaidi China yashikiria msimamo wake wa 'uwazi kwenye biashara'

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uchina inasema iko wazi kwa biashara – je hili linaweza kuaminiwa?

Wakati mkutano wa kila mwaka wa bunge la China ukifikia tamati baada ya wiki yenye shughuli nyingi za mikutano, pengo kubwa linatanda katika ajenda ya mwisho ya Jumatatu.

Bunge la Kitaifa la Watu wa China hukatishwa na mkutano wa Waziri Mkuu na waandishi wa habari. Lakini mwaka huu, na kwa muda uliosalia, mambo yamebadilika.

Maafisa wamesema hakukuwa na haja ya mkutano na wanahabari ikizingatiwa kulikuwa na fursa nyingine ya wao kuuliza maswali. Lakini waangalizi wengi waliona hii kama ishara nyingine ya uimarishaji na udhibiti, katika kile kilichokuwa mada ya mkutano wa Bunge, hata kama viongozi wakuu walizungumzia uwazi.

Kufutwa kwa mkutano na waandishi wa habari kunapunguza wasifu wa Waziri Mkuu Li Qiang. Ingawa tukio hilo lilipangwa, ilikuwa nafasi adimu kwa wanahabari wa kigeni kuuliza maswali na kumpa kamanda wa pili wa nchi hiyo nafasi ya kukaza misuli yake.

Katika miaka ya nyuma, kulikuwa hata na matukio ambayo hayakutarajiwa. Kwa mfano, mnamo 2020, Waziri Mkuu wa wakati huo Li Keqiang alifichua takwimu ambazo zilizua mjadala juu ya madai ya serikali kwamba ilikuwa imeondoa umaskini.

Kile kilichoonekana kama kufifia kwa uangalizi wa Waziri Mkuu, pamoja na kongamano fupi mwaka huu, zote ni dalili za mabadiliko ya kimuundo yanayoendelea ndani ya Chama cha Kikomunisti cha China (CCP) ambapo Rais Xi Jinping anazidi kujilimbikizia madaraka kwa gharama ya watu binafsi na taasisi, alibainisha Alfred Wu, profesa msaidizi katika Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Singapore ambaye anasomea utawala wa China.

Lakini kwa ulimwengu wa nje, chama hicho kina nia ya kutoa taswira ya aina tofauti huku kikipambana na kupungua kwa imani ya wawekezaji wa kigeni na kuzorota kwa jumla kwa uchumi wake.

Akihutubia wanahabari wa kimataifa wiki jana, waziri wa mambo ya nje Wang Yi alisisitiza kuwa China bado ni sehemu ya kuvutia kuwekeza na kufanya biashara.

"China inasalia kuwa na nguvu kama injini ya ukuaji. 'China ijayo' bado ni China," alisema, kabla ya kutaja njia ambazo "China inafungua mlango wake kwa upana zaidi."

Mwongozo wa kiuchumi wa mwaka huu, uliotolewa na Bw Li mwanzoni mwa kikao, uliweka mipango ya kufungua maeneo zaidi kwa uwekezaji wa kigeni na kupunguza vikwazo vya upatikanaji wa soko katika sekta kama vile viwanda na huduma.

Hatua hizi zimekuja baada ya wawekezaji wa kigeni kutishwa na sheria za hivi majuzi za kupinga ujasusi na ulinzi wa data, pamoja na kuzuiliwa kwa ghafla kwa wafanyabiashara wa China na wa kigeni. Uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni nchini China hivi karibuni ulipungua sana.

"Kuna ukaguzi mdogo wa kisiasa na usawa, hakuna uwazi. Hili ndilo jambo kubwa zaidi kwa wawekezaji... huwezi kutabiri kitakachotokea, kwa hivyo unaepuka hatari," alisema Dk Wu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live