Rais Samia ameshuhudia utiaji saini wa mikataba mikataba na makubaliano ya kimkakati 15 akiwa pamoja na Rais wa China, Xi Jinping ambapo miongoni mwa mikataba hiyo ni kuhusu mahitaji ya kuwepo na soko kubwa la usafirishaji wa maparachichi kutoka Tanzania kwenda China,
Mkataba mwingine uliotiwa saini ni unaohusu msaada wa RMB milioni 100 za ushirikiano wa kiuchumi na kitaalamu baina ya nchi hizo mbili vilevile, kumetiwa pia saini makubaliano kuhusu mahitaji ya kuwepo na soko kubwa la usafirishaji wa Mabondo ya Samaki pamoja na bidhaa nyingine za uvuvi kutoka Tanzania kwenda China.
China inaongoza kwa uwekezaji nchini Tanzania hadi kufikia Mwezi Oktoba 2022, Jumla ya miradi 1,098 yenye thamani ya Dola za Kimarekani Bilioni 9.6 ilisajiliwa katika kituo cha uwekezaji cha TIC, miradi hiyo imezalisha ajira 131,718.