Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

China kufadhili miradi ya kimkakati nchini

January Makamba Kuongoza Usalama Bomba La Mafuta China kufadhili miradi ya kimkakati nchini

Mon, 20 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

China imesema itaendelea kufadhili miradi mipya ya kimkakati ya Tanzania inayoendelea, baada ya kuridhishwa na utekelezwaji ya miradi ya awali.

Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Misaada la China (CIDCA), Luo Zhaohui, ameyasema hayo kwenye mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Januari Makamba yaliyofanyika jijini Beijing, China.

Zhaohui amesema kuna uwezekano mkubwa kwamba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anaweza kusaini mikataba mipya ya ushirikiano na misaada Septemba mwaka huu pembezoni mwa mkutano wa Wakuu wa Nchini na Serikali wa Jukwaa la Ushirikiano wa China na Afrika (FOCAC) ambao amealikwa tayari.

CIDCA ndiyo taasisi inayopitisha misaada na mikopo ambayo serikali ya China kutoa kwa nchi zote duniani na Waziri Makamba alikwenda kufanya mazungumzo na mkuu huyo ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi inayoendelea nchini China.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live