Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

China kuanzisha kiwanda cha pikipiki za umeme Zanzibar

Pikipiki Umeme China kuanzisha kiwanda cha pikipiki za umeme Zanzibar

Wed, 23 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) imeeleza kuwepo kwa nia ya Wawekezaji kutoka Jamuhuri ya Watu wa China ambao wanalengo la kuwekeza Zanzibar katika Sekta ya Kilimo pamoja na Uwanishwaji wa Kiwanda cha Kutengeneza Pilipiki zinazotumia Nishati ya Umeme.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamalaka hiyo ZIPA Sharif Ali Sharif wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kufuatia Kikao Kazi baina Ujumbe kutoka china na Watendaji wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika Ukumbi wa Hotel ya Goldern Tulip Kiembe samaki Mjini Unguja.

Amesema kuwa, Ujumbe wa Watu wa China upo Zanzibar kufuatia Ziara ya Rais Dkt Hussein Ali Mwinyi nchini humo na kuwaomba wawekezaji mbalimbali kuja kuwekeza Zanzibar.

Amesema, miongoni mwa maeneo ambayo wamelenga kuwekeza ni kilimo hasa katika zao la muhogo ambalo kufuatia mpango huo zao hilo litaingia kwenye sehemu ya zao la mkakati ambapo nchini China limekuwa linahitajika kwa kiwango kikubwa.

Aidha Mkurugenzi Sharif amesema kwamba, Aidha amesema kupitia ujumbe huo tayari wapo wawekezaji ambao wamedhamiria kuekeza kwa kuanzisha kiwanda cha utengenezaji wa Honda za Umeme hali itakayosaidia kuimarisha uchumi wa Zanzibar.

"Ziara ya Dkt Mwinyi Nchini imepelekea kupokea Ujumbe mkubwa wa Watu kutoka China ambapo wanania ya kuwekeza katika Sekta ya Kilimo hususani katika zao la Muhogo ambapo sisi tutaliwekea zao hilo katika mazao ya kimkakati," ameeleza.

"Hata hivyo Ujembe huu umeonesha nia ya kuanzisha kiwanda kikubwa cha kutengeneza Pikipiki zinazotumia Nishati ya Umeme," Ameongeza.

Amefafanua kuwa Uwekezaji huo utasaidia kwa kiasi kikubwa kufungua fursa mbalimbali za Ajira kwa Vijana sambamba na kukuza Uchumi wa Zanzibar.

Nae mwakilishi wa ujumbe huo kupitia kampuni ya Tanzania commodity commerce Investment inayofanya kazi ya kuzitangaza bidhaa za Ttanzania nchini China John Rwehumbiza amesema wawekezaji hao wamelenga kuwekeza katika kilimo cha muhogo na maharage ya soya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live