ChatGPT ambayo imekuwa gumzo kwa siku za hivi hivi karibuni imefungua rasmi huduma za ChatGPT Plus nchini Tanzania ambapo mteja atapata huduma hata wakati kukiwa na watumiaji zaidi.
Vilevile, mtumiaji atapata kipaumbele katika vipengele vipya vitakavyokuwa vikitolewa. Hata hivyo huduma hiyo itakuwa ikipatikana kwa shitariki ya dola 20 kwa mwezi karibu Sh 45,000.
Kwa ilivyokuwa huduma za ChatGPT zilikuwa zikipotea kulingana na ongezeko la watumiaji hatahivyo mtengenezaji huyo amesema sasa ChatGPT itapatikana kwa kasi kwa wale watakao kuwa wakitumia ChatGPT Plus.
Kampuni hiyo kwa sasa inasiwa kwa kufanya mapinduzi katika teknolojia ya AI. OpenAl ilianzisha chatbot yake, inayojulikana kama ChatGPT, mwezi Novemba 2022. Wiki iliyopita, kampuni ya Google ilizindua bidhaa mpya inayoitwa “Bard” ikiwa ni mpango wa kushindana na ChatGPT, chatbot yenye akili ya hali ya juu (AI) katika mfumo wa kompyuta na intaneti.
Sundar Pichai, Mkurugenzi Mtendaji wa Google na kampuni mama ya Alphabet, alisema katika chapisho kwamba Bard imefunguliwa kwa watu wachache “wanaoaminika” kama majaribio kuanzia Jumatatu, na mipango ya kuifanya ipatikane kwa umma "katika wiki zijazo," inaendelea.
Kama vile ChatGPT, ambayo ilitolewa hadharani mwishoni mwa Novemba na kampuni ya utafiti ya AI OpenAI, Bard imejengwa kwa mtindo mkubwa wa lugha. Miundo hii imefunzwa kwenye hifadhi nyingi za taarifa mtandaoni ili kutoa majibu ya kuvutia kwa vidokezo vya watumiaji.