Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Channel za kitaifa kuonekana kwenye ving'amuzi vyote bila malipo

A702c703f6651a7632586cfc8128c424 Serikali kufanya marekebisho kuruhusu chaneli za kitaifa visimbuzi vyote

Thu, 26 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SERIKALI inaandaa kanuni mpya za leseni, utangazaji na maudhui mtandaoni ambazo zitaruhusu chaneli za kitaifa ambazo zipo kwenye kundi la ‘Free to Air Channels’ kuonekana katika visimbuzi vyote bila malipo ya mwezi.

Kwa sasa chaneli kama ITV, Channel Ten, Clouds na Star TV hazipatikane katika visimbuzi vya huduma kwa malipo, (Pay TV) kama vile Dstv na Zuku.

Afisa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Philip Njombe amesema moja kati ya mapendekezo ya marekebisho ya kanuni nikurusu chaneli za kitaifa kuonekana katika visimbuzi vya Pay TV bila malipo.

Amesema Pay TV pia zitapata idhini ya kurusha matukio mbashara, jambo ambalo mwazo lilikuwa limezuiliwa. Vilevile Pay TV zitaruhusiwa kuanza kupokea matangazo lakini kwa kiwango kitakacho dhibitiwa na Mamlaka.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk Jim Yonazi amesema serikali inakusudia kuweka mfumo mzuri utakaosaidia sekta ya habari ambayo itaiwezesha Tanzania kuwa nchi ya mfano Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ya kukusanya maoni ikiwemo Rasimu ya Marekebisho ya Kanuni za Maudhui Mtandaoni za Mwaka 2020 pamoja na Kanuni za Maudhui ya Utangazaji katika Radio na Television za Mwaka 2018, Dk Yonazi amesema serikali imepokea maoni mengi.

“Tunataka Wananchi wafaidi na kunufaika na huduma hizi,” amesema Naibu Katibu Mkuu nakusisitiza hii haitakuwa mara ya kwanza kwa kuwa wakati wa mabadiliko kutoka analogia kwenda digitali, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekuwa kinara katika kusaidia na kufundisha nchi zingine.

Chanzo: www.habarileo.co.tz