Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Changamoto za umeme kuwa historia

Umeme 1 660x384 Changamoto za umeme kuwa historia

Fri, 28 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MKURUGENZI Mtendaji wa shirika la umeme nchini (TANESCO), Maharage Chande amesema katika kuongeza ufanisi uwajibikaji na utendaji wa kazi Shirika la Umeme nchini TANESCO, wamedhamiria kumaliza changamoto ya umeme ifikapo mwezi June 2024. - Mkurugenzi huyo ameitoa kauli hiyo leo Julai 27, 2023 Dar es Salaam katika mkutano wa shirika hilo na wahariri wa vyombo vya habari na kusema changamoto ya umeme nchini itabaki kuwa historia kutokana na kukamilika kwa mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere litakalochangia uzalishaji umeme kwa wingi ambapo kwa sasa ujenzi wake umefikia asilimia 90 hadi kukamilika kwake. - Aidha Mkurugenzi huyo amesema shirika hilo lina mpango wa kuja na mita janja ili kupunguza mchakato mrefu wa ulipaji umeme. - "Mita janja zitawezesha mtu kuingiza umeme na sio lazima awe nyumbani kwake popote pale alipo anaweza kuingiza umeme, tulianza tathimini ya kuhama mfumo kutoka mfumo tuliopo sasa na kwenda kwenye mfumo mpya wa mita janja na matokeo ya tathimini hiyo yalishatoka. - zipo mita janja ambazo tunazijaribu na zinafanya kazi licha ya kwamba tumepata changamoto ya gharama kubwa ya matumizi yake , kwasasa tunaanagalia njia mbadala ambayo itapunguza gharama kwa watumiaji wetu" amesema Chande -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live