Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Changamkieni fursa sekta ya utalii

Sekta Binafsi Ni Mdau Wa Uchumi Na Maendeleo   Dk. Hussein Mwinyi.jpeg Changamkieni fursa sekta ya utalii

Wed, 21 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amewataka wananchi kuchangamkia fursa mbalimbali za sekta ya utalii ikiwemo ajira, kuuza mazao wanayozalishwa nchini na usafirishaji.

Mwinyi amesema hayo alipofungua Mkutano wa pili wa Kimataifa wa sekta ya utalii na Maonesho "The Z Summit 2024" katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, uwanja wa ndege Zanzibar tarehe: 21 Februari 2024.

Aidha amesema Serikali itaendelea kujenga miundombinu ya ujenzi wa barabara mpya, kuboresha usambazaji wa umeme na maji pamoja na viwanja vya ndege.

Ameongeza kusema kuwa Sheria mpya ya uwekezaji Zanzibar ya mwaka 2024 imeweka vivutio vingi ambavyo vinalinda uwekezaji na kuwa vivutio vya kodi Afrika Mashariki.

Kwa upande mwingine Mwinyi amesema Pemba ni chachu ya ukuaji wa uchumi na maendeleo ya baadae kwa kuanzishwa ukanda wa uwekezaji wa Pemba (PIZ) ili kuvutia wawekezaji na kuchochea shughuli za kiuchumi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live