Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Changamkieni fursa kwenye madini

Mud Matope Madini Changamkieni fursa kwenye madini

Tue, 21 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

WATANZANIA wametakiwa kuchangamkia fursa zilizopo katika uwekezaji katika sekta ya madini ili kuupiga jeki uchumi wa taifa kwa kutengeneza ajira na walipa kodi wapya.

Hayo yamesemwa jana Mei 20, 2024 na Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Mhandisi Yahya Samamba ikiwa bado siku mbili kufanyika kwa Jukwaa la Tatu la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini ambalo litaanza rasmi kesho kutwa Mei 22, 2024 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Arusha International Conference Centre (AICC).

Mhandisi Samamba amesema kuwa, kuna fursa nyingi katika Sekta ya Madini kutokana na mazingira bora yanayowavutia wawekezaji hivyo kuwataka watanzania kuchangamkia fursa hizo.

“Watu wajitokeze kwa wingi siku ya jukwaa ili kubaini fursa zilizopo katika sekta hii ya madini na kuzichangamkia,” amesema Samamba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live