Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amemtaka Meneja wa Soko la Feri, Denis Mrema kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake abuni vyanzo vipya vya kuongeza mapato.
Pia amemtaka kupitia upya sheria zilizopo kwa kushirikisha wafanyabiashara, ili kupunguza kero kwa wafanyabiasha hao.
Chalamila amesema hayo alipotembelea soko la Feri na moja ya changamoto aliyokutana nayo ni soko hilo kukabiliwa na idadi kubwa ya wafanyabiashara zaidi ya 3000, huku uwezo wake halisi ni kuhudumia wafanyabiashara 1500 hadi 2000 tu.
Amesema Rais Samia ana nia njema na wafanyabishara hao wa soko la Ferina na kuwataka kila mmoja anayefanya biashara katika soko hilo kuwa mlinzi wa mwenzie, ili idadi ya wafanyabishara iliyopo sasa ya zaidi 3,000 isiongezeke, hadi pale serikali itakapofanya maboresho ya soko.
Chalamila amesema amebaini uholela wa wafanyabishara, kukosekana kwa uaminifu miongoni mwa wafanyabishara kupitia kiwango cha mapato ambacho kinatakiwa kipatikane, ubovu wa miundombinu, sheria sio shirikishi hivyo ni wakati muafaka wa kuanza kupangana.