Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chalamila ashtukia upigaji soko la Zakhiem, asitisha uzinduzi

Albert Chalamila RR Chalamila ashtukia upigaji soko la Zakhiem, asitisha uzinduzi

Tue, 29 Aug 2023 Chanzo: Mwananchi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila, amesitisha uzinduzi wa Soko la Mbagala Zakhem baada ya kubaini uwapo wa madalali waliochukua fedha za watu kwaajili ya kuwauzia vizimba. Kufuatia taarifa hizo, Chalamila ametoa wiki moja na kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama, kufanya uchunguzi Ili kuwabaini. Hatu hiyo inakuja ikiwa ni wiki moja tangu alipotangaza kuunda kamati ya kuchunguza masoko yote, kwa kile alichoeleza vipo vikundi vya watu wanaojimilikisha masoko na kukusanya fedha kutoka kwa wafanyabiashara.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila, amesitisha uzinduzi wa Soko la Mbagala Zakhem baada ya kubaini uwapo wa madalali waliochukua fedha za watu kwaajili ya kuwauzia vizimba. Kufuatia taarifa hizo, Chalamila ametoa wiki moja na kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama, kufanya uchunguzi Ili kuwabaini. Hatu hiyo inakuja ikiwa ni wiki moja tangu alipotangaza kuunda kamati ya kuchunguza masoko yote, kwa kile alichoeleza vipo vikundi vya watu wanaojimilikisha masoko na kukusanya fedha kutoka kwa wafanyabiashara. Amesema ziara alizozifanya kwenye baadhi ya masoko alibaiani Kuna upotevu wa mapato, ikiwemo baadhi ya watu kukodisha vizimba na kukusanya fedha. Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jana Jumatatu Agosti 29, 2023 katika viwanja vya Mbagala Zakhiem, aliwataka madalali wote waliochukua fedha kuhakikisha wanazirudisha. "Nilikuwa nizindue hili soko leo, nalisimamisha kwa wiki moja, kwa kuwa wapo watu ‘waliodaka’ fedha za watu kuna timu inaundwa Kwa kushirikiana na Mkurugenzi na vyombo vya ulinzi na usalama,"amesema. "Nitawanyoosha kwenye utawala wangu hayo mambo hayapo, kama Kuna dalali yoyote amechukua fedha za wafanyabiashara warudishe,"amesema Chalamila. Alibainisha kuwa soko hilo lililogharimu zaidi ya sh 2 bilioni lina maduka 150 lakini wafanyabiashara waliotuma maombi ni zaidi ya 2000. "Nitakapokamilisha uchunguzi nitahakikisha bei ya pango inaenda na hadhi ya soko, nitatoa utaratibu kuhakikisha makundi yote wanapata nafasi wakiwemo walemavu na vijana,"ameongeza. Akizungumza katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mobhare Matinyi amesema, katika mwaka wa fedha 2022/2023 jumla ya sh 152 bilioni zilitolewa kwaajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo. Amesema kati ya fedha hizo Sh43 bilioni ziliekekezwa kwenye barabara, Sh 61 bilioni miradi ya umeme, Sh15 bilioni miradi ya maji, Sh 7 bilioni kwenye elimu ya msingi na Sh10 bilioni shule za sekondari.

Chanzo: Mwananchi