Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chalamila apiga 'stop' madalali soko la Zakheim

Chalamila: Viongozi Wa Dini Muiombee Serikali Chalamila apiga 'stop' madalali soko la Zakheim

Thu, 23 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amesema Serikali inaendelea kuboresha masoko yote na kuendeleza ujenzi wa masoko mapya ili kutoa fursa za kukuza maendeleo kwa Wakazi wa mkoa huo.

RC Chalamila ametoa kauli hiyo katika ufunguzi wa soko jipya la kisasa la Zakheim lililopo Mbagala, ambalo ujenzi wake umegharimu Shilingi Bilioni 2.4.

Akifungua Soko hilo, Mkuu wa mkoa Albert Chalamila, ametoa mwezi mmoja kwa wafanyabiasha kuhakikisha wanaanza biashara haraka ndani ya soko hilo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sixtus Mapunda amewataka Wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao kwenye barabara ya mwendokasi kuacha mara moja kabla hatua kali hazija chukuliwa na mamlaka ya Wilaya hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live