Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chalamila afika soko la samaki Feri

Chalamila Samaki Feri.png Chalamila afika soko la samaki Feri

Wed, 16 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amekagua soko la samaki Feri Jijini Dar es Salaam na kuongea na Wafanyabiashara ambapo amesema amebaini wanafanya biashara kiholela, kukosekana kwa uaminifu miongoni mwao, ubovu wa miundombinu na sheria isiyokuwa shirikishi.

RC Chalamila amesema huu ni wakati muafaka kwa Wafanyabishara kupangwa vizuri na pia Meneja kuwa na ubunifu zaidi katika kuongeza mapato vilevile kupitia upya sheria zilizopo kwa kuwashirikisha Wafanyabishara wenyewe.

“Bado kuna uholela kila mmoja haelewi yuko wapi baadaye yanaibuka maugomvi kwahiyo ili lazima tuje tuendelee kupangana upya ili angalau kusiwe kuna migogogro ya mara kwa mara jambo la pili ambalo nimeligundua baadhi yetu sio wa kweli kwenye mapato yanayotakiwa kuingia hapa”

RC Chalamila ameagiza pia kupunguzwa kwa matumizi ya mkaa katika soko hilo ambayo huzalisha moshi na kuwataka kuanza matumizi ya gesi “Ule moshi pale nafikiri mmepata malalamiko unakwenda moja kwa moja kwa Waziri Mkuu unakwenda mpaka Ikulu Watu wetu hawa wanatumia mkaa soko kama hili leo mkaa sio mwafaka kwasababu ya mabadiliko ya Tabia ya Nchi ni vizuri gesi ikatumika”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live