Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chadema: Mawakala wa mbolea ya ruzuku wawafuate wakulima

Mbolea 1 Chadema: Mawakala wa mbolea ya ruzuku wawafuate wakulima

Tue, 22 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati msimu wa kilimo ukianza nchini, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimewataka mawakala wa usambazaji mbolea za ruzuku kupeleka mbolea hizo maeneo ya vijijini waliko wakulima tofauti na kuwataka wakulima wasafiri hadi wilayani kufuata mbolea hiyo.

Wito huo umetolewa jana Jumatatu Novemba 21, 2022 na Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Bunge la Wananchi la chama hicho, Sijaona Karoli jijini Mwanza wakati ambao wakulima wanatakiwa kufuata ruzuku hizo kwa mawakala na wasambazaji wanaopatikana maeneo ya wilaya nchi nzima.

Karoli amesema kutendo cha kuwataka wakulima wadogo wafuate mbolea wilayani kitasababisha wengi wao kulima bila tija kutokana na kuogopa kutumia gharama kubwa na muda mwingi kufuatilia mbolea hiyo.

"Mvua za masika zinaendelea kunyesha wakulima tayari wamepanda mazao hasa mahindi bila kupata mbolea ya kupandia aina ya DAP hii maana yake ni kwamba mazao ya wakulima kwa msimu huu yanaweza kuharibika na hivyo kusababisha taifa kuingia kwenye wimbi la njaa," amesema Karoli

Ametaja mpango huo wa kuweka mbolea mjini utafanya wakulima wadogo wasipate fursa ya kununua mbolea ya ruzuku na kutoa fursa kwa wataomudu kusafiri kwenda mjini kununua mbolea hiyo kuwauzia walioshindwa kumudu kwa bei kubwa.

"Kama inavyifahamika wakulima wengi wanalima eneo dogo tu, uhitaji wake unaweza kukuta ni mifuko 10 tu sasa huyu unamwambia asafiri hadi wilayani ambapo nauli yenyewe tu ni gharama ya huyo mbolea, nafikiri watendaji wa wizara watafakari hili na kuchukua hatua," amesema

Ameongeza; "wanashindwa nini kama Serikali kupeleka vituo vya mbolea kila kata ya nchi hii ili wakulima wadogo wawe na distance (umbali) mfupi wa kufuatilia, kasi na mawakala waongezwe, uwazi utawale ili kuboresha kilimo Tanzania kwa mbolea ya ruzuku na tuongeze uzalishaji wa chakula."

Kwa upande wake, Mkulima wa Bustani kata ya Nyaguge wilayani Magu mkoani Mwanza, Renatus Mhangwa amesema utaratibu huo ni changamoto kwani wakulima wadogo wanapopokea ujumbe kwa njia ya simu kuwa wamechaguliwa kuchukua mbolea hiyo hushindwa kufanya hivyo kutokana na maduka inapotolewa kuwa mbali.

Mhangwa amesema mkulima akishindwa kwenda kuichukua, mbolea hiyo huishia kuneemesha mawakala wa waliokasimiwa jukumu la kuuza mbolea hiyo huku mazao yakiharibika shambani.

Ametoa mfano kuwa gunia lenye ujazo wa kilo 50 la mbolea ya kupandia (DAP) wilayani Magu linauzwa Sh 60,000 huku ya kukuzia ikiuzwa Sh 70,000 huku mkulima akitakiwa kuingia gharama ya kuisafirisha hadi kijijini lilipo shamba lake.

"Nafikiri kuna umuhimu serikali iiitazame hili suala upya, kuna uwezekano msimu ujao kusiwe na chakula cha kutosha kwa sababu wakulima wanalima bila mbolea tutarajie hata mavuno yatapungua kama hatua za haraka hazitachukuliwa wakulima wadogo wafikishiwe mbolea waliko," amesema Mhangwa

Chanzo: www.tanzaniaweb.live