Dar es salaam. Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI) limeipongeza Serikali ya Tanzania kutokana na bajeti ya mwaka 2019/20 ya Sh33.1 trilioni iliyowasilishwa Alhamisi iliyopita ya Juni 13, 2019 kusikiliza kilio chao.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Juni 17,2019 Mkurugenzi Mtendaji wa CTI, Leodeger Tenga amesema bajeti hiyo itasaidia ukuaji wa viwanda hapa nchini na kukuza masoko ya bidhaa ndani na nje ya nchi.
"Tunaishukuru serikali kwa bajeti hii imesikiliza na kuzingatia maoni yetu tuliyopendekeza kupitia wizara ya fedha ili kufikia adhima ya Tanzania ya viwanda 2020 na uchumi wa kati mwaka 2025" amesema Tenga
Amesema baadhi ya maeneo yaliyozingatiwa ni pamoja na kupunguza wingi wa vyombo vya udhibiti na tozo 54 ambavyo vilikuwa vikwazo vikubwa katika mazingira ya kufanya biashara nchini.
“Kwa kitendo cha serikali kuongeza kodi za uingizwaji wa bidhaa na kuondoa/kupunguza tozo za malighafi za ndani, itasaidia kukuza na kulinda viwanda na masoko” amesema
Tenga ameongeza kuwa jambo lingine lililowafurahisha ni kuanzishwa kwa ofisi ambayo itasikiliza maswala ya kodi katika wizara ya fedha ambapo kama mtu hajaridhika na hesabu za makadirio ya kikodi kutoka Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) anaweza kwenda kueleza na ukasikilizwa.
Pia Soma
- Wapinzani Tanzania waja na bajeti ya Sh 29 trilioni, vipaumbele vitano
- Profesa Kabudi, Dk Mpango watakiwa kujiuzulu
- Kamati ya Bunge yaridhishwa kauli ya Mpango 2018/19 kuhusu ETS
“Tunaishauri serikali kuboresha fani katika ufundi ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi Zaidi,” amesema Zavery.