Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CTI  yaanzisha mfumo wa taarifa kwa wanaotaka kuwekeza

7ba23d4326ab0cde4c127e6c00dbfa54 CTI  yaanzisha mfumo wa taarifa kwa wanaotaka kuwekeza

Wed, 16 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

SHIRIKISHO la Wenye Viwanda Nchini (CTI) limezindua mfumo utakaowarahisishia wafanyabiashara na wawekezaji kupata taarifa muhimu wanapotaka kuwekeza na utawawezesha kujua fursa mbalimbali zinazopatikana ndani na nje ya nchi.

Uzinduzi wa mfumo huo uitwao Manufacturers Information Portal ulifanyika jana jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Profesa Riziki Shemdoe.

Akizungumza mara baada ya kuzindua mfumo huo, Profesa Shemdoe alisema mfumo huo utawasaidia wafanyabiashara na wawekezaji wa kutoka nje ya nchi na wale wa ndani kupata taarifa muhimu kwa urahisi wanapotaka kuwekeza tofauti na ilivyokuwa awali.

Alishauri CTI kuutangaza mfumo huo ili wafanyabiashara wengi na wawekezaji wajue namna ya kuingia na kupata taarifa muhimu, badala ya kuhangaika kwenda wizarani na kwenye taasisi za umma kutafuta taarifa za uwekezaji.

“Huu mfumo unapatikana dunia nzima utakuwa msaada mkubwa kwa wafanyabiashara kupata taarifa, tunachotakiwa kufanya ni kuutangaza kwa nguvu kuhakikisha watu wengi wanaujua na wautumie kupata kile wanachotaka,”alisema.

Alisema serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji kuvutia uwekezaji zaidi kutoka ndani na nje ya nchi na kuhakikisha uhusiano mzuri uliopo baina ya sekta ya umma na binafsi unaendelea kuimarika ili kukuza mazingira ya baishara.

Mwenyekiti wa Kwanza wa CTI, Paulo Makanza alisema waliamua kuanzisha mfumo huo kuwarahishia wafanyabkiashara na watu wanaotaka kuwekeza kupata taarifa muhimu sehemu moja ya nini cha kufanya na hatua za kuchukua

“Si watu wote wanajua wanatakiwa wafanye nini au wawe na kitu gani wanapotaka kuwekeza sasa mfumo huu utakuwa jibu kwao kwa sababu wakiingia tu wataelimishwa hatua zote wanazotakiwa kuchukua, zamani ilikuwa lazima uzunguke kwenye wizara na taasisi za umma,” alisema.

Chanzo: habarileo.co.tz