Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CTI wataka fedha miradi ya maendeleo ziongezwe

Tue, 19 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Shirikisho la wenye viwanda Tanzania (CTI) limeishauri Serikali kuongeza pesa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeldo hadi kufikia asilimia 40 ya bajeti yote au zaidi ili kuchochea uzalishaji katika uchumi wa viwanda.

Wito huo umetolewa leo Juni 18 na Mwenyekiti wa CTI, Dk Samwel Nyantahe ikiwa ni siku chache tangu kusomwa kwa mapendekezo ya bajeti ya mwaka 2018/2019 ambapo Serikali imepanga kukusanya na kutumia Sh32.47trilioni.

Katika bajeti hiyo Sh20.468 trilioni ambayo ni sawa na asilimia 63 itatumika katika matumizi ya kawaida huku Sh12 trilioni sawa na asilimia 37 ikielekezwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo kama umeme, barabara, reli na bandari.

Dk Nyantaje amesema kuongezwa kwa fedha katika utekelezaji wa miundombinu itakuwa ni chachu ya kuongeza uzalishaji, kuboresha mazingira ya biashara na kusaidia sekta ya viwanda kuchangia katika ukuaji wa uchumi.

"Tusiwe tu tunakusanya hela ili tutumie bali tukusanye hela ili tuziweke katika matumizi ya miradi ya maendeleo," amesema Dk Nyantahe.

Amesema katika bajeti hii mambo mengi ambayo walikuwa wakiyapigia kelele kama shirikisho la viwanda yamefanyiwa kazi jambo ambalo linawahamasisha kama wazalishaji.

"Kama wadau bajeti hii tunaipa asilimia 70 kwa sababu kodi na tozo nyingi tulizokuwa tunazipigia kelele zimeondolewa tunaipongeza sana Serikali," amesema Dk Nyantahe

Chanzo: mwananchi.co.tz