Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CTI: Tunataka bidhaa za ndani kushindana kimataifa

Bidhaa Za Vijana CTI: Tunataka bidhaa za ndani kushindana kimataifa

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi Mtendani wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI), Leodgar Tenga amesema lengo la shirikisho hilo ni kuhakikisha wazalishaji wa ndani wanazalisha bidhaa ambazo zitashindana katika masoko ya kimataifa.

Akizungumza katika maonesho ya kwanza ya kimataifa ya wazalishaji wa ndani yanayofanyika mkoani Dar es Salaam, Tenga amesema ongezeko la wazalishaji wa ndani limewasukuma wao na TanTrade kuandaa maonesho hayo.

Zaidi ya wazalishaji wa ndani 100 wanashiriki maonesho hayo ya siku tatu kwa lengo la kuonesha bidhaa zao na teknolojia mbalimbali katika uzalishaji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live