Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CRDB yazindua mfumo kutoa maoni kwa QR Code

18623 Pic+crdb CRDB yazindua mfumo kutoa maoni kwa QR Code

Tue, 14 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benki ya CRDB imezindua mfumo wa kimtandao wa ukusanyaji na utoaji maoni QR Code utakao muwezesha mteja kutoa maoni yake moja kwa moja hadi ngazi husika kupitia simu ya mkononi (simu janja).

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mtandao wa Matawi, Bonaventura Paulo wakati wa uzinduzi huo kwa ngazi ya mkoa uliofanyika katika Benki ya CRDB Mwanza.

Amesema kuwa mfumo huo utawezesha mteja kupata urahisi wa kufikisha maoni yake kwa ngazi husika muda huo huo pasipo kupitia kwenye mikono ya mtu.

"Tupo hapa kuzindua kampeni ya kukusanya maoni kwa mfumo wa kidigital mwanzo tulikuwa tunatumia maboksi ya maoni ambao ulikuwa unachukua muda mrefu kufika katika eneo husika lakini sasa mfumo huu utasaidia kutoa maoni na mrejesho ya mteja kwa muda mfupi"amesema Paulo.

Ameongeza kuwa mfumo huo utamsaidia mteja kutoa maoni yake juu ya tawi lingine na utarahisisha kupokea maoni,maboresho ,malalamiko na kushughulikia changamoto kwa wakati ili kuongeza ufanisi ili aweze kufarahia huduma za CRDB sambamba na kupata huduma zingine.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja kutoka benki hiyo Yolanda Urio, amesema lengo la kuanzisha mfumo huo ni kuhakikisha wateja wanapata huduma iliyo bora na inayotakiwa hivyo kila mara wataendelea kuboresha namna ya kuendelea kupokea maoni kutoka kwa wateja wanaotumia simu janja kwani mfumo huo ni rahisi na waharaka zaidi.

"Namna ya kutoa maoni unafungua kamera unaielekeza palipo na bango la Qr Code ,moja kwa moja itakupeleka katika tovuti ya maoni ya wateja wetu na hapo unaweza kuchagua tawi ambalo unataka kutoa maoni hakika huduma hii italeta mabadiliko makubwa na hakutakuwa na ucheleweshaji wa utoaji majibu" ameeleza Urio.

Naye Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitta amesema kutokana na thamani kubwa walionayo wateja wao aliwasihi kuchangamkia fursa na kuiona huduma hiyo ni yao kwani itawasaidia kupata ufumbuzi wa changamoto zao kwa wakati muaafaka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live