Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CRDB yakabidhiwa cheti utoaji wa huduma ya bima

CRDB Yakabidhiwa Cheti Utoaji Wa Huduma Ya Bima.jpeg CRDB yakabidhiwa cheti utoaji wa huduma ya bima

Thu, 18 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamishna wa bima nchini Dkt Baghayo Saqware amekabithi cheti cha utoaji wa huduma ya bima kwa Benki ya CRDB ikiwa ni benki ya kwanza hapa nchini kupata cheti hicho kama kampuni tanzu kuanzisha huduma hiyo .

Akikabithi cheti hicho, Kamisha Dkt Bahgayo Saqware amesema kuwa, anataka kuona benki hiyo inafanya kazi katika ubunifu wa hali ya juu na kuacha kufanya kazi kwa mazoea ikilinganishwa na Taasisi zingine ambazo zimekuwa zikifanya kazi kwa mazoea.

Aidha amesema kuwa, kitendo cha benki hiyo kukidhi vigezo na kukabithiwa cheti hicho ni mfano wa kuigwa na taasisi zingine kwani uwepo wa bima hiyo utasaidia sana kutoa huduma za bima kwa wanachama wake na kukuza Pato la taifa

Aidha amesema kuwa, benki ambayo inatoa huduma zake kimataifa ikiwemo nchi ya Congo,Burundi,na Tanzania ni vizuri ubunifu uliotumika katika nchi hizo utumike kukuza sekta hiyo ya bima.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dk Abdul Majid Nsekela amesema kuwa, amefurahishwa sana kupata cheti hicho kama benki ya kwanza hapa nchini.

Nsekela amesema kuwa,mbali na kuanza kama mawakala wanajivunia kuona wamekuwa kampuni rasmi ya kutoa huduma ya Bima ambapo amesema wao watajiongeza kuhakikisha wanafikia makundi yote maalumu.

Aidha ametaja makampuni ambayo yatanufaika ni pamoja na wasafarishaji,wakulima ,wafugaji, viwanda ,ambapo huduma hizo zitakuwa zinatolewa kwa njia ya kidigitali ili kufikia walengwa waliokusudiwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa bima ya CRDB, Wilson Mzava amesema kuwa,wapo tayari kuwahudumia watanzania kuanzia sasa ambapo wateja wao wategemee utofauti mkubwa endapo watapata majanga ya aina yoyote matarajio kampuni hiyo kulipa kwa haraka zaidi ili waweze kuona tofauti.

Aidha ameongeza kuwa, Watanzania kuanzia sasa watarajie kuwepo kwa matawi hayo katika benki ya CRDB pamoja na mawakala kwa ajili ya kupata huduma hiyo ambayo inapatikana nchi nzima.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live