Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CRDB kuwekeza nje ya nchi, yataja sababu

Uchumi Kupanda CRDB kuwekeza nje ya nchi

Thu, 29 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

UTAFITI , ubunifu na udhutubu umewezesha Benki ya CRDB kuwekeza nje ya nchi ikiwemo uboreshaji wa huduma kidigitali sanjari na historia ya Tanzania katika kudumisha amani iliyopo.

Akizungumza na wanahabari leo Agosti 29, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela amesema uboreshaji wa utendaji wa kazi ikiwemo kujiimarisha kimtaji, kutoa huduma bora pamoja na kutawanya mtandao huo nchini ni sababu za uwekezaji huo.

"Usimamizi bora wa bodi ya CRDB pamoja na uboreshaji wa huduma za ndani umepelekea benki kufanya utafiti wa soko na kwenda baadhi ya nchi za EAC na wamezipanga kulingana na vipaumbele vyao na nchi ya Burundi walienda kwa mara ya kwanza kama kuanza kutoka huduma za kibenki na leo hii wamekuwa watoa huduma bora zaidi,” amesema Nsekela.

Akizungumza katika kikao kazi cha wenyeviti wa bodi na watendaji wakuu wa taasisi za umma nje ya ukumbi wa Kituo Cha Kimataifa cha Mikutano cha (AICC) Arusha kilichoandaliwa na Msajili wa Hazina, Nehemia Mchechu, Nsekela amesema kikao kinatoa taswira kwa taasisi kujitafakari kwani sio lazima uende nje ya nchi peke yako bali ni wakati sasa mashirika kukaa kibiashara.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live