Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CRDB, Visa kuzindua malipo kwa simu za mkononi

KIMEI TZW

Thu, 7 Jun 2018 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kuzindua programu yake na Tigo, kampuni ya Visa sasa imejipanga kushirikiana na Benki ya CRDB kutoa huduma zake kwa kutumia simu za mkononi (mVisa). Ushirikiano huu wa pili utakuwa wa aina yake baada ya benki hiyo kuzindua kadi za mkopo kwa ajili ya wateja wake mapema mwaka huu.

Mkurugenzi mtendaji wa CRDB, Dk Charles Kimei anasema wataendelea kuwa wabunifu ili kukidhi mahitaji yanayobadilika kila siku kutokana na maendeleo ya teknolojia. “Muda si mrefu tutazindua programu maalumu itakayowawezesha wateja wetu kufanya malipo kwa kutumia simu za mkononi popote duniani badala ya kadi za kutolea fedha,” alisema Dk Kimei.

Kwa sasa wateja wa benki hiyo wanapata huduma kupitia zaidi ya matawi 250 yaliyopo nchini, vituo vya mauzo (PoS) na mawakala. Kimataifa, kadi za mkopo za benki zinafanikisha miamala ya aina tofauti huku zikitoa fursa ya kukopa mpaka Sh100 milioni kwa njia ya mtandao. Mpango wa kuzindua program hiyo utatoa fursa kwa wateja kufanikisha malipo ya aina tofauti bila haja ya kubeba fedha taslimu au kutembea na kadi (ATM).

Kwenye hafla hiyo, CRDB iliwatangaza wateja watatu watakaoenda kushuhudia ufunguzi wa michuano hiyo huku 12 wakijishindia luninga na ving’amuzi vya DSTv vyenye kifurushi cha miezi miwili kitakachowapa fursa ya kutazama michuano hiyo mwanzo hadi mwisho. “Malipo kwa njia ya mtandao ni muafaka zaidi kwa wateja wetu na wauzaji wa huduma na bidhaa pia. Inaondoa ulazima wa kutafuta chenji na uwezekano wa kuvamiwa,” alisema Dk Kimei.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live