Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CRDB: Hatuna mpango wa kufunga tawi la Chato

44142 Crdbpic CRDB: Hatuna mpango wa kufunga tawi la Chato

Wed, 27 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Benki ya CRDB imesema haina mpango wa kufunga tawi lake la Chato mkoani Geita.

Benki hiyo imetoa kauli hiyo kufuatia taarifa za uongo zinazosambaa mitandaoni zikieleza uwepo wa mpango wa kulifunga tawi hilo la kisasa lililofunguliwa Machi 9,2018 na Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatano, Febuari 27, 2019, Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa CRDB, Tully Mwambapa amesema hawana mpango wa kufuta tawi hilo.

“Hivi karibuni, kumetokea wimbi la taarifa za uzushi kuhusu benki yetu zikiwa na lengo la kuiharibia benki yetu kibiashara na taswira yake katika jamii,” amesema Mwambapa.

Amesema CRDB haina mpango wa kufunga tawi hilo na huduma zinaendelea kutolewa kama kawaida tangu tawi hilo lilipofunguliwa.

“Kwa yeyote anayefanya haya mambo anafanya uharibifu kwa CRDB pamoja na nchi yetu ya Tanzania kwani benki yetu ni muhimu sana katika uchumi wa Tanzania,” amesema Mwambapa.

Soma Zaidi: Rais Magufuli kuzindua tawi la benki Chato



Chanzo: mwananchi.co.tz