Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CMSA kuwanoa watoa huduma za sekta ya masoko ya mitaji na dhamana

12935 Pic+mauzo TanzaniaWeb

Tue, 21 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Mamlaka ya masoko ya mitaji na Dhamana (CMSA) kwa kushirikiana na Taasisi ya mafunzo ya masoko ya mitaji na uwekezaji ya nchini Uingereza (CISI) wamezindua mpango wa kuendesha mafunzo endelevu ya kitaaluma (CPD) kwa watoa huduma wa sekta hiyo nchini.

Katika uzinduzi wa mpango huo uliofanyika leo Agosti 20, ofisa mtendaji mkuu wa CMSA Nicodemus Mkama amesema lengo ni kuimarisha uwezo na kuwajengea ufanisi watoa huduma.

Pia, amesema ni utekelezaji wa itifaki ya soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki linalotaka watoa huduma katika sekta hiyo kupatiwa mafunzo yanayotambulika kimataifa na kufaulu mitihani.

"Mpango huu unaweka utaratibu na vigezo vya ushiriki katika soko la mitaji mpaka kufikia mwaka 2020, atakayeruhusiwa kupewa leseni ya kutoa huduma ni mtu ambaye atakuwa amehudhuria mafunzo endelevu kwa walau saa 10 kwa mwaka. Hiki kitatumika kama kigezo cha utoaji wa leseni za watoa huduma  ambaye hatakidhi hatopewa leseni," amesema Mkama.

Mkama amesema washiriki wa masoko ya mitaji ambao tayari wanaleseni watatakiwa kufanya mafunzo endelevu na kutekeleza mipango inayotekelezwa na CMSA. "Utaratibu huu unaiweka Tanzania katika nafasi nzuri ya kwa kuwa na wataalamu wanaokidhi viwango vya kimataifa,".

Muwakilishi wa CISI  Kevin Moore anasema mafunzo endelevu kwa watoa huduma yatasaidia kuongeza ufanisi lakini bia ubunifu na kukuza biashara zao.

"Lakini nikumbushe tu mafunzo haya hayataleta mabadiliko kwa siku moja na siyo kwamba yatabadilisha kitu kilichokibaya kuwa kizuri bali kizuri kitakuwa kizuri zaidi," amesema Moore.

Chanzo: mwananchi.co.tz