Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CMCA yatoa tahadhari ya upatu haramu

Pic Fedha Data Wastaafu CMCA yatoa tahadhari ya upatu haramu

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) imeitaka jamii kujihadhari na upatu haramu, kwani ni hatari kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.

Meneja Uhusiano wa CMSA, Charles Shirima ameyasema hayo leo Novemba 22,2023 jijini Arusha alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya wiki ya huduma za fedha kitaifa.

Shirima amesema jamii ijihadhari na matapeli wanaoahidi watu kuvuna pesa nyingi kirahisi.

Amesema wameamua kutoa elimu kwa wajasiriamali kwani upatu haramu umewaathiri wengi kutoka kada hiyo nchini kwa kujiingiza kwenye mikopo harama ikiwamo kausha damu.

"Kutokana na hali hiyo Watanzania wanapaswa kujiinga kwenye masoko ya mitaji kwani ni sehemu ya mfumo wa sekta ya fedha unaowezesha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kugharamia shughuli za maendeleo ya muda mrefu yaani mwaka mmoja," amesema.

Amesema fedha za maendeleo hupatikani kwa kuuza hisa, hatifungani za kampuni na vipande katika uwekezaji wa pamoja.

Mchambuzi wa fedha mwandamizi wa CMCA, Witness Gowelle amesema kupitia maadhimisho hayo wametoa elimu kwa wajasiriamali mbalimbali ili kuwajengea uwezo zaidi.

Nayem, mjasiriamali wa kutoka wilayani Ngorongoro, Sas Kotete amesema wajasiriamali wengi wameathirika kupitia upatu haramu hivyo elimu waliyoipata itawasaidia kuepukana na hayo.

Mjasiriamali mwingine wa mkoani Arusha, Naini Losusu ameipongeza CMSA kwa kuwapa elimu hiyo kwani inawajengea uwezo zaidi juu ya upatu haramu.

Maadhimisho ya wiki ya huduma za fedha kitaifa kupitia kauli mbiu ya elimu ya fedha, msingi wa maendeleo ya uchumi, yanafanyika jijini Arusha, kwa siku sita ambapo yalianza Novemba 20 na yatafikia tamati Novemba 26 mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live