Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CEO wa benki ya TADB karipoti kazini,amewataja wakulima kwenye mikopo

Nyabu Mkurugenzi MKuu wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo TADB Frank Nyabundege.

Fri, 13 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo TADB Frank Nyabundege amewataka wafanyakazi, kufanya kazi kwa weledi ili wakulima wa Tanzania waweze kunufaika na benk hiyo.

Akiwa katika makao makuu ya benki hiyo jiji Dar es Salaam, Bwn. Nyabundege ambaye ameteuliwa hivi karibuni na Rais Samia aliwaambia wafanyakazi katika benki hiyo kuwa asilimia 70% ya Watanzania wanajihusisha na kilimo, hivyo kuna kila sababu ya kuwapatia elimu wakulima juu ya shughuli zinazofanywa na benki hiyo kwa kuboresha maisha yao na kuwapatia mikopo nafuu.

"Ni matumaini yangu, Tutafanyakazi kwa weledi na ufanisi mkubwa ili kufikia malengo ya kimfumo yaliyopo kwenye kilimo, ufugaji na sekta ya uvuvi. kwa upande wangu nitaongeza bidii na kuhakikisha tunafikia malengo" Anasema Nyabundege.

Pamoja na mambo mengine aliwataka wafanyakazi kufanya kazi ya ziada kwa kutoa Elimu ya huduma zinazotolewa na benki hiyo ili kuonyesha umuhimu wake kwa kuwaletea wakulima manufaa ya moja kwa moja.

Lengo kuu la Benki ya TADB ni kuisaidia serikali kwa kuwawezesha wakulima katika maeneo matatu,Kuongeza uzalishaji, Kuanzisha viwanda na kutengeneza ajira kwa wasio na ajira.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live