Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CAG afichua upigaji mabilioni ya Pride

KICHERE CAG afichua upigaji mabilioni ya Pride

Mon, 4 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), amebaini ubadhirifu wa mabilioni ya shilingi na mali za Kampuni ya Ukuzaji wa Juhudi za Maendeleo Vijijini (PRIDE).

Katika ripoti yake ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha 2018/19, CAG Charles Kichere, anafafanua kuwa, Pride ni kampuni iliyoanzishwa Mei 5, 1993 kuhamasisha maendeleo vijijini kupitia mradi wa maendeleo vijijini.

Anasema mradi huo unaendeshwa kwa ubia kati ya Serikali ya Kifalme ya Norway na Serikali ya Tanzania; na kwamba kuanzia mwaka 2015, ulitokea mgogoro juu ya umiliki wa Kampuni ya Pride kati ya Serikali ya Tanzania na wakurugenzi wa kampuni.

CAG anasema mgogoro ulihitimishwa kwa maagizo ya mahakama na makubaliano ya wakurugenzi wa kampuni kukubali kuwa kampuni ya Pride ni mali ya serikali.

"Kufuatia makubaliano haya, Januari 4, 2019, Wizara ya Fedha na Mipango na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), iliiomba ofisi yangu kufanya ukaguzi wa kuhakiki mali na madeni ya kampuni hadi kufikia Oktoba 31, 2019 na kutathmini iwapo kulikuwa na ubadhirifu uliosababishwa na uwapo wa mifumo duni ya usimamizi katika uendeshaji wa kampuni kwa kipindi cha kuanzia Januari Mosi, 2017 hadi Desemba 31, 2019.

"Ukaguzi wangu ulibaini idadi ya mali na madeni ya kampuni hadi kufikia tarehe 31 Oktoba 2019, na uligundua uwapo wa ubadhirifu wa mali na madeni ya kampuni," anabainisha.

CAG anafafanua kuwa kampuni ina jumla ya mali zenye thamani ya Sh. bilioni 19.97 hadi kufikia Oktoba 31, 2019 zinazojumuisha mikopo ya wateja ya Sh. bilioni 8.82 na mikopo ya watumishi wake Sh. bilioni 11.14.

"Ukaguzi wangu juu ya uhalali na ukamilifu wa mali ulibaini kuwa mali zilizotajwa hazikuwa timilifu na kulikuwa na ubadhirifu kwenye mikopo iliyotolewa.

"Kampuni ya Pride ina utaratibu wa kutoa mikopo kwa watumishi wake ikiwa ni sehemu ya motisha ya utumishi. Hadi kufikia tarehe 31 Oktoba 2019, kampuni ilikuwa inawadai watumishi wake kiasi cha Sh. bilioni 11.14. Mikopo hii ilikuwa kwenye makundi matatu, ambayo ni mkopo wa nyumba, mkopo maalum, na mkopo wa jumla.

"Ukaguzi wangu wa mifumo ya usimamizi wa mikopo (DUX) na usimamizi wa fedha (Bankers Realm) ulibaini kuwa, kiasi cha mikopo ya Sh. milioni 745.59 kinatokana na mikopo ya watumishi 168 walioacha au kuachishwa kazi, ambapo kampuni haina mkakati wowote wa namna ya kurudishwa kwake.

"Mikopo yenye thamani ya Sh. bilioni 10.38 ilitolewa kwa watumishi 33 bila makato ya urejeshaji kufanyika kwenye mishahara yao. Vilevile, ukaguzi uligundua mikopo yenye thamani ya Sh. bilioni 2.6 ambayo haikuwa na taarifa za wakopaji na hivyo kushindwa kujumuishwa kama sehemu ya mali za kampuni," anabainisha.

CAG anasema upungufu huo ulitokana na uwapo wa mifumo duni ya usimamizi katika kampuni na vitendo vya kibadhirifu vya watumishi waovu.

Ukiachia mikopo ya watumishi na wateja, CAG anasema ripoti ya mwisho ya mkaguzi wa nje ya mwaka wa fedha unaoishia Desemba 31, 2016, inaonyesha kampuni inamiliki mali zingine zinazojumuisha mali zisizohamishika, mali zinazohamishika za kudumu, hisa za kampuni, dhamana za muda mfupi na mrefu, pamoja na mali za kudumu zisizoshikika.

Hata hivyo, CAG anasema mali hizo hazikujumuishwa kwenye orodha ya mali za kampuni hadi kufikia Oktoba 31, 2019 kwa sababu mbalimbali kama vile hisa za uwekezaji zenye thamani ya Sh. bilioni 2.31 katika Benki M (Tanzania) zilizopotea baada ya benki hiyo kufilisika; dhamana za muda mrefu za Sh. bilioni 48.2 katika Benki za CRDB, Benki M (Tanzania) Limited, na NMB zilizotumika kulipia madai ya mikopo katika benki hizo.

Zingine ni mali zisizohamishika (Sh. milioni 942.11); na mali za kudumu zisizoshikika (Sh. milioni 956.46). CAG anasema mali hizo zote hazikuripotiwa kwa kuwa rejista ya mali haikuainisha gharama za mali moja moja, badala yake ikawekwa tarakimu moja ambayo ukaguzi wake ulishindwa kuthibitisha uhalali na usahihi wake.

"Kipande cha ardhi chenye viwanja namba 1 & 2 vyenye hati Na. 392106 katika Kitalu A mkoani Morogoro chenye thamani ya Sh. bilioni 1.44 hakikuripotiwa kwa kuwa thamani yake ya wakati wa ukaguzi (Januari 2020) haikujulikana.

"Ninapendekeza kuwa hatua za kisheria na kinidhamu zichukuliwe kwa watumishi waliohusika katika ubadhirifu wa mikopo ya wafanyakazi. Pia, mthamini wa mali wa serikali afanye tathmini kujua thamani ya mali ambazo hazikujumuishwa kama mali za kampuni kwenye ripoti hii," anashauri.

CAG pia anasema, ukaguzi wake ulibaini kampuni ilikuwa na madeni ya jumla ya Sh. bilioni 130.11 hadi kufikia Oktoba 31, 2019 na kwamba, wakati wa kutathmini ukamilifu na uhalali wa madeni yaliyotambuliwa, aligundua madeni matano kati ya saba ya madeni toka taasisi za fedha za nje ya nchi kutoka Stromme Foundation, Incofin, Responsibility, NMI Fund III KS, na Symbiotics yenye jumla ya Sh. bilioni 47.68, hayakuwa yamesajiliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live