Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CAG abaini matumizi makubwa Magogoni

Magogoni Matumizi CAG abaini matumizi makubwa Magogoni

Wed, 20 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere imebaini matumizi makubwa ya mafuta katika kivuko cha Magogoni yenye thamani ya Sh410.95 milioni.

Ripoti hiyo ya mwaka unaoishia Juni 30,2021 tayari iliwasilishwa bungeni wiki iliyoipita inaeleza Kanuni ya 277 (4) ya Kanuni za Fedha za Umma za 2001 inataka matumizi ya mafuta yalinganishwe na matarajio ya kawaida ya aina ya usafirishaji au mtambo, ili kutambua utumiaji uliozidi kiasi ambao unaweza kuashiria ama hitilafu ya kiufundi au upotevu wa mafuta.

Hivyo Kichere alisema katika uchunguzi wake alibaini kuwa kituo cha kivuko Magogoni kinaendesha vivuko vitatu.

“Uchambuzi wangu juu ya usimamizi wa mafuta kwa mwaka wa fedha 2020/21 ulionyesha kulikuwa na matumizi makubwa ya mafuta, ambapo jumla ya lita 178,673 za dizeli sawa na Sh410.95 milioni zilitumiwa zaidi ya mahitaji ya kawaida,” alisema.

Kichere alisema ingawa Wakala wa Ufundi wa Umeme (Temesa) ilikanusha uwepo wa matumizi makubwa ya mafuta katika kituo kwa madai kuwa mara nyingi mashine (injini) zinafanya kazi kati ya uzito wa asilimia 75 hadi asilimia 90 badala ya asilimia 50 (ambayo uchambuzi wangu ulitumia).

Hata hivyo, ukaguzi wangu ulionesha mashine (injini) zinafanya kazi kwa asilimia 75 hadi 90 wakati wa foleni, ambapo ni asubuhi (saa 1 hadi 4 ) na jioni (11 hadi 2 usiku). Wakati kwa zaidi ya saa 17 (mchana na usiku wa manane) injini zinafanya kazi hata chini ya uzito wa asilimia 50.

Advertisement Alisema matumizi makubwa ya mafuta yanaweza kuwa yamesababishwa na kasoro za mitambo au udhaifu wa usimamizi wa mafuta kituoni, jambo linaloiweka wakala katika hatari ya matumizi makubwa ya fedha kugharamia uendeshaji wa vivuko.

Alipendekeza Temesa ipitie na kuboresha mfumo uliopo wa udhibiti wa ndani unaosimamia matumizi ya mafuta kwenye vituo vya feri.

Taasisi 15 zakacha mifuko hifadhi ya jamii

Katika hatua nyingine, ripoti hiyo ya CAG imebaini taasisi 15 ambazo hazikuwasilisha makato ya mishahara kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii yenye thamani ya Sh391.68 milioni.

Ripoti hiyo imebaini fedha hizo hazijawasilishwa katika Mfuko wa Pensheni kwa Mashirika ya Umma (PSSSF) na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jami (NSSF), Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Alisema kwa maoni yake kutowasilisha makato kwenye mifuko hiyo na taasisi nyingine za umma kunasababishwa na kutokuwa na utaratibu mzuri wa uwasilishaji wa makato hayo kwa wakati.

Kichere alisema kutowasilisha makato kunaathiri watumishi kwa kuwasabishia kutopata haki na faida zinazotokana na kujiunga na mifuko ya jamii na afya.

Pia alisema taasisi zilizoshindwa kuwasilisha makato kwa wakati zinaweza kupata adhabu, hivyo kulipa malipo yasiyo na tija na kupata hasara.

Alisema alibaini kutolipa kwa wakati makato hayo katika taasisi sita zimelazimika kulipa adhabu ya Sh491.51 milioni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live