Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CAG abaini mapingamizi ya kodi ya bil 102.6/- kutotatuliwa

D2bbee04099bebb0787d6769757b9065 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), Charles Kichere

Mon, 25 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2020/21 imebaini kuwapo kwa mapingamizi 155 ya kodi yenye thamani ya Sh bilioni 102.6 ambayo hayajatatuliwa.

Amesema mapingamizi hayo hayajapatiwa ufumbuzi kwa zaidi ya miezi sita kama inavyoelekezwa katika mkataba wa huduma kwa mlipakodi wa Julai, 2017.

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere alisema mapingamizi hayo yalisajiliwa katika idara za kodi za ndani na uchunguzi wa kikodi yakiwa na miezi saba mpaka 124 wakati wa ukaguzi.

Alisema kucheleweshwa kwa utatuzi wa mapingamizi ya kodi kunaathiri malengo ya ukusanyaji wa kodi kwa kuwa yanafunga kiasi kikubwa cha kodi.

Kichere alisema katika uchunguzi wake pia aligundua hakuna uthibitisho wa malipo ya amana ya pingamizi wala msamaha wa kodi uliotolewa na kamishna kwa kulipa kiwango kidogo cha 1/3 ya Sh bilioni 4.65 kabla ya kusajili pingamizi kama matakwa ya sheria yanavyotaka.

“Naishauri serikali kwa kuchukua hatua stahiki kushughulikia mapingamizi ya kodi mapema kwa kuongeza idadi ya wafanyakazi wenye uwezo na ujuzi katika kitengo cha huduma ya kiufundi na kitaalamu na kuongeza mafunzo ya ndani na kuimarisha ukokotozi wa kodi,” alisema Kichere.

Aliishauri serikali kuhakikisha mapingamizi yote ya kodi yanasajiliwa baada ya kulipa 1/3 ya kodi au kiasi cha kodi kisicho katika pingamizi chochote kilichojuu zaidi, vinginevyo kamishna awe amesamehe pale ambapo vigezo vya kufanya hivyo vinakuwapo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live