Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bwawa la Kidunda kuja na faida lukuki

Kadunda Bwawa Bwawa la Kidunda kuja na faida lukuki

Wed, 31 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

akati mradi wa Bwawa la Maji la Kidunda ukianza kutekelezwa mkoani Morogoro, fursa lukuki za kiuchumi zinatarajiwa kupatikana kutokana na miradi itakayoambatanishwa katika ujenzi wa bwawa hilo.

Mbali na uhakika wa upatikanaji wa maji, utekelezwaji wa mradi huo utaambatana na ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 101 na uzalishaji wa megawati 20 za umeme.

Mradi huo unaotekelezwa na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) unatarajiwa kuwa na uwezo wa kuhifadhi maji yatakayotumika kwa miaka mitatu mfululizo.

Hayo yalielezwa jana na Kaimu Ofisa Mtendaji wa Dawasa, Kiula Kingu alipowasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Morogoro.

Mradi huo utakaogharimu Sh335 bilioni, alisema ujenzi wake utaambatana na ujenzi wa barabara hiyo, uzalishaji wa umeme, kadhalika utatoa fursa ya shughuli za uvuvi kwa wananchi wa maeneo ya karibu na mradi.

“Ujenzi wa mradi huu utaenda kuleta uhakika wa upatikanaji wa maji kwa muda wote kwa mwaka mzima, pia kuzalisha umeme katika bwawa la kidunda wa megawati 20 zitakazoenda kuingia katika gridi ya taifa na kutunza mazingira kwa viumbe hai,” alisema.

Mbali na faida hizo, Kingu alisema bwawa hilo litakapokamilika litakuwa na uwezo wa kuhifadhi maji kipindi cha masika, yatakayotumika nyakati za kiangazi.

Uwezeshaji wa mitambo ya Ruvu juu na chini kuwa na maji ya kutosha hasa nyakati za kiangazi ni moja ya mambo yaliyotajwa na Kingu kuwa sababu ya utekelezaji wa mradi huo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mporogoro, Rebeca Msemwa pamoja na kuipongeza Dawasa, aliitaka jamii kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali.

“Tunajivunia utekelezaji wa mradi huu katika Mkoa wetu wa Morogoro, Serikali imedhamiria kuhakikisha upatikanaji wa maji kwa kipindi chote cha kiangazi hivyo hatuna budi kuunga juhudi hizi kwa kuhakikisha Dawasa inatekeleza mradi huu kwa ukamilifu,” alisema.

Naye Mkurugenzi wa Bonde la Wami Ruvu, Mhandisi Elibariki Mmasi alisema kinachofanywa nao ni kuhakikisha vyanzo vya maji vinavyoingia katika bwawa hilo vinahifadhiwa ili visiathiriwe na shughuli za binadamu.

"Tumejipanga kufanya uthamini na tathmini katika maeneo yote yanayozunguka chanzo cha mto Ruvu na kutangazwa kuwa maeneo ya uhifadhi kwa kutenga Sh4 bilioni ili kuhakikisha bwawa la Kidunda linatoa suluhu ya upatikanaji wa maji kwa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani," alisema.

Mradi huo unatarajiwa kuanza kutekelezwa Juni 18, mwaka huu na utekelezwaji wake utafanyika kwa miaka mitatu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live