Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bunge lazuia POSTA kuhodhi usafirishaji virushi, lataka kuwe na ushindani

POSTA TANZANIA Bunge lazuia POSTA kuhodhi usafirishaji virushi, lataka kuwe na ushindani

Fri, 3 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria imeyakataa mapendekezo ya Serikali ya kulitaka Shirika la Posta Tanzania peke yake kuwa na mamlaka ya kusafirisha vifurushi vyenye uzito wa kuanzia gramu 500 (nusu kilo) hadi kilo 10.

Akiwasilisha maoni ya kamati hiyo kuhusu Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali namba nne, mwenyekiti wa kamati hiyo, Najma Giga amesema wanapinga hilo kwa sababu maudhui yake hayaendani na misingi ya soko la ushindani linalotakiwa kuwa huru.

Amesema utekelezaji wake utaleta changamoto na kuathiri ajira za kundi kubwa la wananchi waliowekeza kwenye sekta hiyo ndogo.

Amesema Serikali ilileta marekebisho yaliyopendekezwa katika Ibara ya 58 kuliruhusu Shirika la Posta kupewa mamlaka ya upekee kuwa chombo pekee cha kusafirisha vifurushi nchini.

“Kamati imekataa kwa sababu maudhui yake hayaendani na misingi ya soko huru hivyo utekelezaji wake ungeathiri ajira za wananchi,” amesema Najma.

Aidha, amesema Serikali haikuwa na uthibitisho wa kujitosheleza kuhusu uwezo wa Shirika la Posta kutoa huduma ya kusafirisha vifurushi kwa utoshelevu unaotakiwa kwa sasa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live