WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), umesema ili kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji nchini ni vyema kujadili kwa pamoja vikwazo vinavyosababishwa na usimamizi wa Sheria, Kanuni na Taratibu zinazotumika na kuangalia jinsi ya kuvikwamua, ili kukuza uchumi wa Tanzania.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Godfrey Nyaisa,alisema hayo mjini Morogoro katika hotuba yake ya ufunguzi wa kikao kazi kati ya Wakala huo na Taasisi za udhibiti wakiwemo Wanasheria na Maofisa wanaohusika na utoaji wa vibali mbalimbali.
Kikao kazi hicho kililenga kujadili mikakati ya pamoja ya namna ya kutatua mikinzano inayojitokeza katika utendaji kazi wa kila siku, kutokana na Sheria, Kanuni na Taratibu zinazozimamia Taasisi hizo hapa nchini.