Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Brela yaelezea changamoto usajili wa kampuni kimtandao

Tue, 6 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Licha ya juhudi za Serikali ya  Tanzania za kurahisisha mchakato wa kusajili  jina la biashara na kampuni hadi kwa njia ya mtandao, Watanzania wengi bado hawafahamu kama wanaweza kutumia simu zao za kiganjani kukamilisha mchakato wa usajili.

Ili kukabiliana na tatizo hilo, Mkurugenzi wa biashara ndogo na za kati kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dk Consolatha Ishebabi akizungumza na Mwananchi jana Jumatano Agosti 5,2019 katika maonyesho ya nanenane mkoani Simiyu alisema Serikali kupitia Wizara na taasisi mbalimbali inatekeleza mpango wa elimu kwa umma kuongeza uelewa wa jamii kuhusu masuala ya biashara na uwekezaji.

"Tumeondoa urasimu na michakato mirefu ya kupata usajili, vibali na leseni ya biashara na uwekezaji."

"Lakini kupitia maonesho haya ya Nanenane, tumebaini Watanzania wengi hawafahamu kuwa wanaweza kusajili jina la biashara na kampuni kupitia simu zao za kiganjani," alisema Dk Ishebabi

Akizungumzia sekta ya kilimo, Dk Ishebabi alisema wizara ya viwanda na biashara kwa kushirikiana na wizara ya kilimo na taasisi mbalimbali za umma na binafsi inatekeleza mikakati ya kilimo chenye tija na uongezaji wa thamani ya mazao.

Mikakati hiyo inahusisha elimu na mikopo kwa wakulima ikiwemo ile zana na pembejeo za kilimo.

Pia Soma

Mmoja wa wakulima waliotembelea banda la wizara ya viwanda na biashara, Johnson Masanja aliiomba Serikali kuhakikisha elimu kuhusu fursa zinazopatikana kupitia sekta ya kilimo inawafikia wakulima hadi ngazi ya vijiji.

Chanzo: mwananchi.co.tz