Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Brela: Watanzania wengi hawajui kutumia mitandao

Brela Wafanyabiashara Brela: Watanzania wengi hawajui kutumia mitandao

Mon, 9 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

OFISA leseni kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) Koyan Aboubakar amesema watu wengi hawana utamaduni wa kufuatilia taarifa za usajili kupitia mitandao yao hali inayofanya kutumia watu ambapo hutoa gharama kubwa au kutapeliwa wakati mwingine.

Akizungumza katika maonesho ya utalii yaliyofanyika Dar es Salaam yajulikanayo kama Swahili Export site, Koyan amesema kupitia maonesho hayo wanatoa elimu kwa wananchi ya namna ya kupata huduma na kutatua changamoto mbalimbali.

“Elimu kwa wafanyabisha bado ni changamoto huduma zetu zinapatikana kwenye mitandao na kwa watanzania wengi kutumia mtandao ni shida huwa wanatumia watu ambao wanarahisisha biashara zao wengine wanatapeliwa au kutoa gharama kubwa sana kupata huduma,”ameeleza.

Amesema wanapopata nafasi kama za maonesho ni rahisi kupata elimu lakini pia kupata huduma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live