Serikali imepokea ujumbe wa wakekezaji kutoka nchini Brazil ambao ni wazalishaji wakubwa duniani katika sekta ya dawa kwenye sekta za afya,uvuvi na mifugo ujumbe ambao umewasili nchini ukiletwa na Balozi wa Tanzania nchini Brazil Adeladus Kilangi.
Kwa mujibu wa Balozi Kilangi wawekezaji hao kutoka Brazil katika kikao cha pamoja na watendaji kutoka taasisi za serikali wameonesha nia ya kujenga kiwanda cha dawa, kuzalisha na kuleta dawa kwenye sekta hizo za afya, uvuvi na mifugo huku mkurugenzi mtendaji wa kiwanda hicho kutoka brazil akieleza nia ya uwekezaji wao nchini.
“Nikiwa nchini Brazili kazi yangu ni kuitangaza Tanzania kusema na wawekezaji wenye nia ya kuja kufanya uwekezajim kwetu sera zetu ni nzuri na hawa jamaa ni kati ya wewekezaji wakubwa kwenye dawa,” alisema balozi Kilangi.
Hata hivyo kwa upande wake mfamasia mkuu wa serikali katika kikao hicho amekiri ukubwa wa wawekezaji hao ambao ni wakubwa katika bara loa america kusini akibainisha kuwa endapo watajenga kiwanda ama kuongeza nguvu kwenye kiwanda cha serikali cha keko itarahisisha huduma na upatikanaji wa dawa nchini.
Kikao hicho kati ya wawekezaji watendaji kutoka taasisi za serikali kimelenga kuwaonesha fursa ikiwa ndiyo azma ya serikali kutangaza sera za uwekezaji nje ya mipaka.