Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Boti ya kitalii yazinduliwa Dar

18599 Pic+boti TanzaniaWeb

Sat, 22 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Jiji la Dar es Salaam linaenda kuwa miongoni mwa majiji makubwa duniani yanayofanya vizuri kwenye utalii wa kuzunguka baharini.

Hilo linakuja kufuatia kuwasili kwa boti ya kifahari ambayo itafanya kazi ya kuzungusha watalii kwenye visiwa vya Mbudya na Bongoyo.

Boti hiyo ya kisasa yenye uwezo wa kubeba watu 60 inaweza kwenda Mafia, Unguja na Pemba visiwani Zanzibar.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa safari za boti hiyo iitwayo Sea Jagura, leo Septemba 21, 2018 Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Tanzania Ocean Cruising, Peter Assanful amesema boti hiyo ni miongoni kwa boti za kifahari Afrika Mashariki.

Amesema boti hiyo ina huduma zote muhimu ikiwemo jiko na sehemu za kupumzikia.

"Ndani ya boti kuna  vyumba vitano vya kulala ambavyo vina uwezo wa kuchukua watu 12 wakalala bila usumbufu wowote."

"Ukiwa ndani unajihisi uko sehemu salama, ndiyo sababu tunasema ni boti ya kifahari, starehe zote utazipata ikiwemo muziki, runinga huku ukiangalia maji, " amesema Assanful.

Amesema pamoja na kufanya biashara, ujio wa boti hiyo unalenga kuchangamsha utalii wa bahari katika Bahari ya Hindi.

Nahodha wa boti hiyo, Aloyce Singano amesema usalama ndani ya boti hiyo ni wa uhakika .

"Niwasihi Watanzania wenzangu waikumbuke pia aina ya utalii, sio kwa ajili ya wageni peke yao hii boti unaweza ukakodi ukafanyia harusi au mkaamua kama kundi iwazungushe."

Chanzo: mwananchi.co.tz