Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Boti mpya kufanya safari Unguja-Pemba

Botu Mpya Mwinyiii (600 X 372) Boti mpya kufanya safari Unguja-Pemba

Wed, 1 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amesema uzinduzi wa boti mpya ya Zanzibar 3 utasaidia kuwepo kwa safari za kila siku kati ya Unguja na Pemba na hivyo kurahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji.

Boti hiyo iliyozinduliwa leo Novemba 01, 2023 na Rais Mwinyi itakuwa ikitumia muda wa saa 2 kusafiri kutoka Unguja hadi Pemba, ikiwa na uwezo wa kubeba abiria 615 kwa mara moja.

Awali usafiri wa Unguja na Pemba ulikuwa unapatikana mara moja kwa wiki na kutumia muda wa zaidi ya saa 4 baharini.

Rais Mwinyi ameanza ziara yake ya siku mbili Pemba, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka mitatu ya uongozi wake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live