Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Boss TRA aapa kuboresha mazingira ya biashara

Tra Boss Boss.png Boss TRA aapa kuboresha mazingira ya biashara

Fri, 9 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuf Mwenda amesema moja kati ya kazi mamlaka yake inaifanya, ni kuhakikisha wanaweka mazingira rafiki ya ufanyaji wa biashara ili kuongeza wigo wa ukusanyaji mapato.

Amesema ikiwa TRA inachangia biashara kufa haitakuwa na tija, kwani makusanyo ya kodi yatapungua na hilo si kusudio la Rais Samia Suluhu Hassan.

"Tutafanya kazi kuhakikisha biashara inakua kwa sababu biashara ikifa sasa sisi tutakusanya wapi kodi? Kwa hiyo sisi TRA kazi yetu ni kurahisisha shughuli za biashara," amesema.

Mwenda amesema hayo leo Ijumaa, Agosti 9, 2024 katika kikao kazi na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine, Mwenda amezindua programu ya TRA Sikika inayomwezesha mtu yeyote kuwasilisha maoni au malalamiko yake kwa kamishna mkuu.

Kuhusu agizo la Rais Samia la kuhakikisha mifumo ya Serikali inasomana, Mwenda amesema tayari wameanza kuyatekeleza na hadi sasa takribani taasisi 80 zimeunganishwa na lengo ni kuunganisha zaidi ya taasisi 300.

"Kwa kweli kufikia mwakani taasisi hizo zitakuwa zimeunganishwa na hili litapunguza sana usumbufu. Na hii itatusaidia kujua nani anafanya nini, yupo wapi na kwa kushirikiana na taasisi zingine tutaweza,"amesema.

Pia, Mwenda amesema miongoni mwa mikakati yake ni kuendelea na ushughulikiaji wa malalamiko ya kikodi ya wafanyabiashara, kusimamia maadili kwa watumishi na wale ambao hawatakubali kubadilika watachukuliwa hatua.

Jambo jingine ni kuongeza umahiri kwa kitengo cha uchunguzi kwa wakwepa kodi na kuchukua hatua stahili dhidi yao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live