Biashara

Habari

Burudani

Michezo

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bosi TPA asema bandari ya Dar iliitwa Bibi Kizee

10654 Bandari+pic TanzaniaWeb

Tue, 3 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari (TPA) Mhandisi Deusdedith Kakonko amesema maboresho yanayofanyika ni kwa ajili ya kurahisisha utoaji wa huduma katika eneo hilo kwani hapo awali, bandari hiyo iliitwa bibi kizee.

Kakonko ameyasema hayo leo Julai 3 wakati wa kongamano la kwanza la wadau wa ndani na nje wanaotumia bandari za hapa nchini lililofanyika jijini hapa.

“Sasa tumeimarisha ulinzi na tunaendelea na upanuzi wa bandari na mengineyo kwa sababu tunataka kutoa huduma za kimataifa hatuwezi kuwachukulia poa wateja. Miaka miwili mitatu nilienda Congo wakaniambia bandari ya Dar es Salaam ni bibi kizee,” amesema Kakonko.

Amesema walimwambia kuwa bibi kizee huyo hata angevalishwa wigi na kupambwa asingeweza kurudia ujana wake lakini wamethubutu na hata mizigo imeongezeka mpaka kufikia tani milioni 16 kwa mwaka (bila kutaja wakati huo ilikuwa kiasi gani) na baada ya ukarabati wa bandari mizigo inayohudumiwa na bandari hiyo itakuwa tani milioni 30.

Mgeni rasmi katika kongamano hilo alikuwa ni Naibu Waziri wa ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye.

Katika mkutano huo, Kakoko amesema maboresho katika huduma sasa ni jambo linalopewa kipaumbele zaidi na mamlaka hiyo hususan wakati huu ambao huduma nzuri kwa wateja na mazingira mazuri ya ufanyaji biashara ndilo jambo la muhimu kuliko mambo yote.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz